Jumanne , 13th Jul , 2021

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa kizimamoto wa Kinondoni Baraza Ali Mvano amewashauri watanzania kutumia nishati mbalimbali kwa usahihi na umnakini ili kuepukana na majanga ya moto.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni Baraza Ali Mvano

Kamishna Baraza amesema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio ambapo ameeleza uwepo wa vifaa vya kung’amua viashiria vya moto nyumbani na ofisini utasaidia kudhibiti majanga ya moto hususan katika kuleta maafa makubwa.

“Mitungi mirefu isikae karibu na jiko ikae nje na wale wanaoishi kwenye chumba kidogo wasiwe wanapikia huko huko, tunashauri kila chumba nyumbani kiwe na smoke dictator (kingamaua moto), sprinkle system (mfumo wa jengo kujizima moto kwa maji),” amesema Kamishna Msaidizi Mvano.

Kamishna Msaidizi Mbando ameongeza kwa kusema kwamba “tunatoaushauri kwa maofisi na ndio maana pia tunaukaguzi wa majengo mapya na ya zamani kabla jengo halijaanza kutumika”.

Akijibu swali kuhusu tukio la moto wa soko la Kariakoo Kamishna Baraza amesema suala hilo lipo kwenye uchunguzi utakapokamilika ndipo ataweza kuliongelea, huku akidokeza chanzo kinachosadikika kusababisha moto katika soko hilo.

“Kwa mfano kama kwenye lile soko la Karikoo pale mpaka kuna  madawa juu ya mbolea na huko ndiko inasadikika ndipo moto ulianza, mpangilio ulikuwa ni mbaya Kariakoo lakini kwa hili wamepata somo naona na uongozi umeamua jinsi ya kuwaweka,” amesema Kamishna Mbando.

Aidha, Kamishna Msaidizi Mvano amekiri kuwa jeshi hilo linahitaji kuongezewa vifaa vya kisasa kwa ajili matukio ya uzimaji moto kutokana na vifaa vilivyokuwepo sasa ni vichache havikidhi mahitaji na havipo katika hali nzuri.