Jumanne , 17th Nov , 2020

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART), imeeleza kuwa, njia ya Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko ya maji hii leo Novemba 17, 2020, kuanzia saa 3:30 asubuhi, na huduma ya mabasi hayo inaendelea kupitia njia ya Kigogo na Mkwajuni.

Eneo la Jangwani

Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 17, 2020, kupitia ukurasa wa Twitter wa Wakala wa mabasi hayo.

"Njia ya Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko ya maji leo, Jumanne, Novemba 17, 2020, kuanzia saa 3:30 asubuhi, huduma ya mabasi ya DART inaendelea kupitia njia ya Kigogo na Mkwajuni ili kufika Kariakoo, Kimara, Morocco, Kivukoni na sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam", imeeleza taarifa hiyo.