
Wito huo umetolewa katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao (Zoom) ukiwakutanisha viongozi hao ambapo kila mmoja alipata fursa ya kueleza mafanikio na fursa zilizopo katika mkoa wake
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema katika mkoa wake kwa sasa hali ya umeme imeanza kuwa imara baada ya mkoa huo kuunganishwa katika gridi ya taifa hivyo wawekezaji wasihofie suala la umeme
"Mkoa wa Kigoma ulikuwa na historia ya kuwa na umeme usio wa uhakika, lakini tunamshukuru sana Rais wetu na hivi ninavyoongea mkoa wa Kigoma umeunganisha na Gridi ya taifa na hii ni wiki ya tatu sasa"
"Ni kweli kuwa kuna wahalifu alienda kuchoma ngozo ya umeme wilaya ya Kakonko, tumeshakaa na wananchi ili kwa pamoja tushirikiane kulinda miundombinu, tunajua ni hamu waliyonayo ya kupata huduma hiyo"
"Kigoma ipo salama pamoja na kuwepo changamoto ya kuwa kimbilio la wakimbizi lakini tumeendelea kushirikiana na mataifa ambayo wakimbizi hao wametokea ili kubadilishana taarifa ambazo zimesaidia sana" amesema RC Thobias Andengenye
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema wawekezaji wasiogope kuwekeza Kagera kwa sababu usalama upo wa kutosha
"Masuala yoyote yanayohusu uwekezaji, watu waje wawekeze Kagera kwa sababu mali zao na uwekezaji wao utakuwa upo kwenye mikono salama chini ya Rais Samia na sisi ambao ametuteua" amesema RC Albert Chalamila
Kwa upande wake Meja Jenerali Suleiman Mzee, ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Mara amewatoa hofu watanzania kuhusu hali ya usalama mkoani humo huku akisisitiza kuwa mkoa huo upo salama kwa ajili ya uwekezaji
"Matukio yanayojitokeza ni ya kawaida, unapokuwa kwenye mkoa mkubwa kama Mara unapopata tukio moja au mawili ambayo yanaashiria uvin jifu wa amani haimaanishi hali ya mkoa haiko salama, kwa ujumla hali ya mkoa wa Mara ni swari"
"Nafikiri mojawapo ya eneo lina rutuba nzuri Tanzania ni wilaya ya Tarime, kule tumeanzisha kilimo cha kahawa nakisisitiza kiendelezwe, tunakusudia mpaka 2025 tufikishe tani elfu 25 - Meja Jenerali Suleiman Mzee, Mkuu wa mkoa wa Mara"