Mtoto akipatiwa matone ya Chanjo
Hatua hiyo ya wazazi kuendekeza imani za kishirika huchangia Vifo vingi kwa watoto na wajawazito na jamii imetakiwa kubadilika kwa kuachana na imani hiyo potofu kwani Chanjo ni kinga ambayo haina madhara.
Hofu hiyo ikawasukuma Muuguzi Mfawidhi wa Kituo hicho, Lyidia Bwanakunu, na wadau wengine wakiwemo mwakilishi wa Serikali za Mitaa Charles Fikiri,na Daktari Nicodemus Rayori, kuwapa elimu ya chanjo mamia ya wazazi na wajawazito waliohudhuria kwenye zoezi hilo utoaji chanjo.
Mkurugenzi wa Kituo hicho, Deogratias Katunzi, amewaondoa hofu hiyo walengwa kwa kusisitiza kuwa aina zote za chanjo kabla ya kuanza kutumiwa huthibitishwa kwanza ubora wake.
Kituo cha Afya Upendo ni Taasisi Binafsi inayoshirikishwa na Serikali kutoa huduma za Chanjo aina zote za kinga kwa watoto, Huduma ya Uzazi wa Mpango na ya Mama na Mtoto bure na serkali imeombwa kuipatia fursa ya unafuu kwa baadhi ya Tozo kutokana na mchango wake.