
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu
Akizungumza katika mahojiano, na Kipindi cha Supa Breakfast, Jesca amesema masuala ya matukio ya ukatili wa kijisia ni masuala mtambuka ambayo yanahusu jamii nzima kiujumla
"Yapo mambo ambayo yanasababisha huu ukatili unaendelea zipo mila potofu kama ukeketaji, mtoto wa kike hawezi kuamua anaamuliwa na wazazi wake, tumekutana na viongozi wa kimila na tumeongea nao na wao wamekubali kuanzia sasa wataanza kutoa elimu na kushirikiana na serikali kupambana na mila potofu" amesema Jesca
Aidha Jesca amesema ili kudhibiti suala hilo zipo sheria za ndoa ambazo inabidi zifanyiwe mabadiliko huku akielezea mikakati wanayoifanya katika jimbo lake kupambana na ukatili wa kijinsia.
"Kikubwa tunachokifanya jimbo la Iringa ni kuhakikisha wadau wote wanaohusika wamehamasishwa vya kutosha na wamepata elimu ya kutosha kujua majukumu yao" amesema Jesca