Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Dorothy Gwajima,
Dkt. Gwajima ameyasema hayo mapema leo Septemba 29, 2021, Jijini Dodoma kwenye mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo amebainishha kuwa baadhi ya mashirika hayatekelezi vizuri maazimio wanayokubaliana hivyo kukiuka taratibu zilizowekwa.
Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima, amezindua mwongozo wa kisera wa mgawanyo wa majukumu yenye kipengele cha kuzuia ukatili wa kijinsia ambapo ameagiza vyombo vinavyolinda na kusimamia haki za binadamu nchini vijitahidi kusaidia makundi yanayokumbwa na manyanyaso mbalimbali.





