Jumatatu , 5th Dec , 2022

Waziri wa Maendeleo ya Jamii  Dkt. Dorothy Gwajima, amezitaka halmashauri zote nchini kufuatilia mienendo ya watoto huku akipiga marufuku uwepo wa madarasa yanayofundisha watoto masuala ambayo ni kinyume na maadili ukiwemo ushoga na kuhakikisha watoto wote wanalindwa.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii  Dkt. Dorothy Gwajima

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga  Waziri Dkt. amesema jukumu la kuwalinda watoto ni la kila mmoja huku akiwataka wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuendelea kupaza sauti.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima akatoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kuandaa mifumo ya pamoja itakayoshirikisha wadau kupata taarifa haraka za ukatili kwa watoto.