Jumatatu , 18th Sep , 2023

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt Pindi Chana, amesema wizara hiyo itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa.

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt Pindi Chana

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia huku akiitaka jamii kushirikiana na serikali kulinda haki za binadamu ikiwemo haki za watoto wanawake na makundi maalum.

Lengo la kampeni hiyo ni kuimarisha upatikanaji wa haki kwa umma na utoaji wa msaada wa kisheria kwa kuzingatia maeneo mbalimbali ikiwemo kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususani haki za watoto na wanawake na kampeni hiyo ilianza Aprili 2023 na tayari imeshafikia jumla ya wananchi 280,000 na wanapata msaada wa kisheria bure.

Awali Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda, amesema mkoa huo umekuwa wa tano kufikiwa na uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo jumla ya wananchi milioni 2.3 wanaenda kufikiwa na huduma hiyo.