Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa hoteli hiyo na kusema kuwa mradi huo unakwenda sambamba na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuimarisha uwanja wake wa ndege ili kuongeza uwezo wake katika kutoa huduma bora kwa abiria na wafanyakazi wa mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi.
"Ujenzi wa hoteli hiyo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 8.5. sawa na sh. bilioni 19.55, ama kwa hakika uwekezaji huu ni mkubwa na naamini wawekezaji hawa wengeliamua kuwekeza katika nchi nyingine yoyote, nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wangelipokelewa kwa mikono miwili" amesema Waziri Mkuu.



