Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Tume hiyo imeundwa hii leo Mei 17, 2023, jijini Dar es Salaam, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo kufanya mgomo na kusitisha kufungua maduka yao kwa ssiku tatu wakilalamikia msururu wa kodi pamoja na kamatakamata.
Tume hiyo imeundwa na wafanyabiashara saba pamoja na viongozi wa serikali ambao inawajumuisha Makatibu wakuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu, Katibu Tawala Ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam pamoja na TRA.
Tazama video hapa chini