Jumanne , 6th Dec , 2016

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mhe. George Simbachawene ameitikia mara moja agizo lililotolewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli la kusitisha zoezi la kuwaondoa machinga maeneo yasiyo rasmi

Waziri George Simbachawene

 

Mhe. Simbachawene, ameitikia agizo hilo kwa kuwataka  wakuu wa wilaya pamoja na halmashauri zote nchini kuangalia ufumbuzi na utaratibu mzuri wa kuwashirikisha wajasiriamali hao ili kupata ufumbuzi ulioshirikisha kuliko utaratibu wa sasa wakuwafukuza bila kusikiliza madai yao.

Mhe. Simbachawene amesema, Rais Magufuli anatambua mchango mkubwa na kazi nzuri inayofanywa na wakuu wa wilaya katika kuleta maendeleo hivyo kuweka maeneo sahihi kwaajili ya wafanyabiashara wadogo kutaleta maana kubwa ya uwajibikaji. 

Hivi karibuni waziri huyu alitoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchi nzima kuhakikisha wanawaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi agizo ambalo lilianza kutekelezwa mara moja katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mwanza na Dar es Salaam.