
Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo leo wakati akiendelea na ziara yake mkoani Kagera ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme.
"Lazima tuwe na Spea sasa hivi sio lazima tusubiri mpaka tatizo litokee ni bora muanze kuagiza mapema Spea ambazo mnahisi hazipo ili linapotokea tatizo la umeme muweze kukabiliana nalo," amesema Dkt. Kalemani.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani yupo mkoani Kagera katika majukumu yake ya kazi ya kukagua miradi ya umeme mkoani humo.