
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki
Kauli hiyo ameitoa alipotembelea na kukagua maendeleo ya kiwanda cha kuchakata maziwa na chakula cha mifugo kilichopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera na kuwahimiza wawekezaji wa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya mifugo nchini kwa sababu inawezekana.
"Niseme tu kwamba sisi Wizara ya Mifugo tuko tayari kumuunga mkono mwekezaji yeyote atakayeweza kufanya uwekezaji mahiri kama alivyofanya Kahama Fresh ili shughuli ya ufugaji iwe ya kibiashara zaidi na kuleta tija kwao binafsi na Taifa kwa ujumla," amesema Waziri Ndaki
Aidha Waziri Ndaki ameongeza kuwa wawekezaji binafsi wakiwekeza katika sekta ya mifugo na kufanya ufugaji wa kibiashara watasaidia kuongeza fursa za ajira kwa wananchi lakini pia watakuza pato la Taifa.