Jumatano , 7th Jan , 2015

Zoezi la kuwaapisha jumla ya wenyeviti 154 wa serikali za mitaa walioshinda katika maeneo mbalimbali manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam limefanyika leo katika ukumbi wa Anatogro, chini ya ulinzi mkali.

Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Bi Hela Mlimanazi leo amewaapisha Wenyeviti wa serikali za mitaa walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika Wilaya ya Ilala uliofanyika hivi karibuni.

Bi Hela amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazowaongoza bila kuingilia ngazi nyingine za maamuizi na kuwatakia ufanisi bora katika utendaji wa majukumu yao

Baadhi ya wenyekiti wa mitaa na wajumbe wao kutoka wilaya ya Ilala wamewataka wananchi wao kushirikiana nao hasa kwenye maswala ya maendeleo kwani jamii nzima inahusika kwa maswala ya maendeleo na isiwaachie viongozi wenyewe kufanya majukumu hayo.

Viongozi hao wameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa kula kiapo cha utumishi huo kwa wananchi waliowapa dhamani kwa kuwapigia kura ya kuwatumika kwa kipindi cha miaka 5.

Ulinzi uliimarishwa katika eneo hilo ili kudhibiti hali yoyote ya uvunjifu wa amani ambao ungeweza kujitokeza, kama hali iliyojitokeza katika manispaa ya Kinondoni siku ya jana.