Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

'Whatsapp' yaiponza shule ya Jangwani

Jumanne , 17th Jul , 2018

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amefunguka na kudai chanzo kikubwa kilichopelekea shule ya sekondari Jangwani kushika mkia kwenye matokeo ya kidato cha sita ni kutokana na wanafunzi hao kujihusisha na uhasherati pamoja na matumizi ya Whatsapp.

Nembo ya mtandao wa kijamii Whatsapp.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo Julai 17, 2018 wakati alipokuwa shuleni hapo na kumuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa shule hiyo kwa kuwa hajaridhishwa na ufaulu wa wanafunzi kwa sababu Jangwani  ndio shule ya ndoto ya wasichana wengi wa kitanzania. 

"Shule ya Jangwani ni shule ambayo yenye upako maalum, sifa na tunu kwa nchi yetu lakini shule hii sasa imekuwa ya tatu kutoka mwisho. Hii ni fedheha ambayo haijawahi kutokea katika shule ya Jangwani. Wanafunzi mmekuja hapa kwaajili ya kusoma sio kwa sketi zenu za rangi ya chungwa, tunataka msome.....

 Kwa taarifa nilizozipata wanafunzi wanatumia simu hizi za Whatsapp na muda mwingi wanaangalia picha zilizokuwa mbovu badala ya kusoma huku wengine wakikalia ku-chat na kuangalia vitu ambavyo sio sawa sawa", amesema Jafo.

Pamoja na hayo, Jafo ameendelea kwa kusema "kwa taarifa nilizozipata hapa za kiuchunguzi ni kwamba wanafunzi wengi wanajihusisha na mambo ya uhasharati, naomba niwaambie endapo mtajihusisha na mambo hayo, elimu haitaweza kuwa rafiki yenu na hilo jambo hata wakubwa wazima linawashughulisha sembuse nyie wanafunzi, nasema kuanzia leo hilo suala lishindwe na ndio maana ufaulu wenu unakuwa mbovu".

Shule hiyo kongwe iliyopo eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam imeingia kwenye nafasi ya 10 shule zilizoweza kufanya vibaya katika matokeo yaliyotangazwa Julai 13, 2018 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).

Shule 10 za mwisho kitaifa ni Jangwani ya mkoani Dar es Salaam, Jang’ombe (Mjini Magharibi), Forest Hill (Morogoro), St James Kilolo (Iringa), Aggrey (Mbeya), Nyailigamba (Kagera), White Lake (Dar es Salaam), Musoma Utalii (Mara), Golden Ridge (Geita) na Ben Bella (Mjini Magharibi).

Huku shule 10 zilizoweza kufanya vizuri zaidi zikiwa ni Kibaha ya Mkoani Pwani, Kisimiri (Arusha), Kemebos (Kagera), Mzumbe (Morogoro), Feza Boys' (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Ahmes (Pwani), St, Mary's Mazinde Juu (Tanga), Marian Girls (Pwani) pamoja na Feza Girls ya Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya