Jumapili , 20th Oct , 2019

Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto imekanusha taarifa ya juu Waziri Ummy Mwalimu anatarajiwa kuzindua duka maalum la linalouza nguvu za kiume, na kusema hakuna dawa iliyothibitishwa na Serikali kuanza kutumika.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo leo Oktoba 20, 2019 imewataka watanzania kupuuza taarifa hizo, na kueleza hazina ukweli wowote.

"Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandaoni mbalimbali ya jamii ikieleza na kumtaja ‘Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Mb), kuzindua duka linalosifika kuuza dawa za kukuza uume hapa nchini’ kuwa hazina ukweli wowote kwani hajawahi kufika au kulifahamu duka hilo." imesema taarifa hiyo
 
"Wizara inawataka wananchi wazalendo kutambua kuwa Serikali ina utaratibu rasmi wa Kiserikali wa kutoa habari na taarifa za viongozi pale wanaposhiriki katika shughuli rasmi za kijamii na utekelezaji wa majukumu ya kisekta katika nyanja zote zinazohusika na sekta hiyo." imeendelea kueleza sehemu ya taarifa hiyo  

Aidha taarifahiyo imesema kuwa kwa kushirikiana na mamlaka za udhibiti madawa, vifaa tiba, vyombo vya dola na usalama hapa nchini, Wizara inaendelea kuwafuatilia wanaotoa taarifa hizi batili na kufanya utapeli kama huu kwetu wananchi na mara watakapobainika watafikishwa katika mkono wa sheria.