Ijumaa , 26th Jun , 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo, amesema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka 2020, wataanza masomo yao rasmi Julai 20, 2020.

Dkt Leonard Akwilapo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Taarifa hiyo kwa umma ameitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema kuwa ratiba hii haiwahusu waliokuwa kidato cha tano wakati shule zinafungwa kutokana na janga la Corona.

"Umma unafahamishwa kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka 2020, wataanza masomo yao Julai 20, 2020, wanafunzi wa Kidato cha 5 watakaoripoti tarehe Juni 29 ni wale waliokuwa Kidato cha 5 wakati shule zinafungwa mwezi Machi" imeeleza taarifa hiyo.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku za hivi karibuni na Waziri wa Wizara hiyo Profesa Joyce Ndalichako, ilieleza kuwa wanafunzi waliopo Kidato cha tano sasa hivi wataanza mitihani yao rasmi Julai 24 na Julai 27, wataingia rasmi kidato cha sita.