Jumanne , 11th Jun , 2024

Rais Samia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda, na kumteua Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa mkoa huo akitoka kuwa Mkuu wa wilaya ya Momba

Dkt Yahaya Nawanda, aliyetumbuliwa

Taarifa ya utenguzi na uteuzi huo imetolewa hii leo ambapo pia amemteua Christopher Magala kuwa Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na anachukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha Rais Samia amemteua George Hillary Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi, Bw. Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani,