Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba
Kauli hiyo ameitoa leo Juni 22, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akijibu hoja za maswali ya msingi yaliyoulizwa na wabunge kufuatia hotuba ya mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 aliyoisoma Bungeni hivi karibuni, na kueleza kuwa miongoni mwa mambo yaliyoleta ukakasi kwa wananchi ni masuala ya vifurushi.
"Kwa wanaoweka muda wa maongezi wa kuanzia 1000 kwenda chini watakatwa sh 5, kwa wanaotumia 7,500 hadi 10,000 watakatwa sh 76, kwa wanaoweka muda wa maongezi wa mwezi mzima kuanzia 10,000 hadi 25,000 watakatwa sh 112 kama anajiunga kwa elfu 50 atakatwa 186," amefafanua Waziri Dkt Nchemba.
Aidha, amefafanua vigezo walivyotumia, "Tumechukua takwimu za watumiaji wa simu tukawaweka kwenye makundi, kuna watumiaji wasiopungua milioni 8 kwa viwango vya mwanzo ambao wana matumizi yasiyozidi 1000, inaenda mpaka kwa wale wanaotumia laki moja na kuendelea ambao wao si wengi".





