Yaliyojiri kesi ya aliyemuuwa mkewe na kumchoma

Jumatatu , 4th Nov , 2019

Kesi ya kuua na kisha kumchoma moto Mke wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, inayomkabili mfanyabiashara Khamis Said, leo Novemba 4, 2019, imeahirishwa hadi Novemba 18, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa jalada la kesi hiyo bado liko kwenye hatua za uchapaji

kwa lengo la kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali Mwanadamizi, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Salum Ally, na kusema kuwa shauri hilo lilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Khamis Said anadaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani, Mei 15, 2019, na kuuchoma moto mwili wa Mke wake huyo na kisha mabaki ya mwili akayabeba na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.