Zahanati
Hali hiyo inawalazimu kwenda umbali mrefu kupata huduma za afya wakati mwingine akinamama wajawazito hujifungulia njiani na wengine kujifungulia majumbani.
Wakazi hao wameiomba serikali kuwatazama kwa ukaribu wananchi hao kwa kuwafungulia Zahanati iliyojengwa kwa nguvu zao na msaada kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu ya tatu, baada ya wananchi hao kuibua mradi huo lakini tangu kukamilka kwake miaka miwili iliyopita bado haujaanza kufanya kazi kutokana na kutokamilika kwa nyumba ya Mganga Mkuu.
Baadhi ya wakazi hao wakapaza sauti zao kwa serikali kuiomba iweze kuwafungulia zahanati hiyo ili waweze kupata huduma jirani na kuepusha vifo.
Mwenyekiti wa Kijiji anaizungumziaje Zahanati hiyo
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha itetemya ameeleza kwa masikitiko makubwa adha wanazopata wananchi wake, akisema kwamba kwa upande wa TASAF wao walishamaliza kazi yao lakini tatizo linaloikwamisha ufunguzi wake bado haijulikani.