Jumapili , 24th Jul , 2022

Zaidi ya watu milioni 50 wanatarajiwa kukabiliwa na viwango vikubwa vya uhaba mkubwa wa chakula mwaka huu katika nchi saba za Jumuiya ya IGAD.

Njaa kuzikumba nchi saba IGAD

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu iliyotolewa leo na IGAD kuhusu Migogoro ya Chakula. Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini na Sudan zinakabiliwa na migogoro mikubwa ya chakula katika kanda hiyo.

 
Karibu watu 300,000 wanakadiriwa kukumbwa na hali mbaya kabisa ya uhaba wa chakula nchini Somalia na Sudan Kusini mwaka huu, huku kitisho cha njaa kikiwa katika maeneo manane ya Somalia mwezi Septemba kama kutakuwa na ukosefu wa uzalishaji wa mimea na mifugo, kupanga kwa gharama za chakla, na kukosekana kwa msaada wa kiutu ulioimarishwa.