Jumanne , 10th Jun , 2014

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC imeonywa kuacha mpango wake wa kutaka kupunguza majimbo ya uchaguzi visiwani humo badala yake wafikirie kuyaongeza au kuyaacha kama yalivyo.

Picha ya eneo mbalo ndio kitovu kikuu cha shughuli za biashara na kiuchumi kisiwani Zanzibar.

Onyo hilo limetolewa na viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria mkutano wa siku moja ulioitishwa na ZEC mjini Chake Chake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Saidi Sodi Said, alisema inashangaza kuona ZEC inajipanga kupunguza majimbo wakati kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu katika maeneo na mitaa kuongezeka.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salimu Jecha, alisema ugawaji wa idadi ya watu , mipaka na majimbo ni jambo la kawaida na lipo kwa mujibu wa sheria ya ZEC, na kuomba ushirikiano wa vyama.