Jumanne , 11th Jan , 2022

Afisa Sheria kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Janeth Mandawa, amesema ni lazima mtoto kupatiwa urithi na mzazi wake ila ikitokea mtoto huyo kafuja mali, hakumhudumia mzazi ama kuzini na mwenza wa mzazi wake basi Baba ama Mama anayo haki ya kumnyima mtoto wake urithi.

Afisa Sheria kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Janeth Mandawa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 11, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, na kusisitiza kwamba hata hivyo mali za mzazi si halali ya mtoto, bali ni hiari ya mzazi kumpa mtoto mali hizo.

"Hautakiwi kutompa urithi mrithi wako halali na ni lazima mtoto umrithishe, isipokuwa kwenye mazingira yafuatayo, mtoto kuzini na mwenza wako unaweza kumnyima, amekufanyia jaribio la kukua, hajakutunza katika shida na maradhi, au ulimpa mali akazifuja, katika mazingira hayo na ikithibitika ni kweli basi huyu hatopata urithi," amesema Janeth.