Jumatatu , 10th Oct , 2016

Mgogoro wa viza baina ya Kenya na Afrika Kusini utakuwa ni miongoni mwa ajenda kuu wakati Rais Jacob Zuma anapowasili Jijini Nairobi hii leo kwa ziara ya siku tatu.

Rais wa Kenya (Kushoto),Uhuru Kenyatta akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Msemaji wa Ikulu ya Kenya Monoah Esipisu amesema jana kuwa Rais Uhuru Kenyatta atatumia ziara hiyo ya Rais Zuma kutaka kuwepo mazingira mazuri ya viza kwa wakenya.

Mapema mwaka huu, Kenya ilikuwa ikishinikiza kuondolewa kwa gharama za sasa za viza zinazotozwa raia wake wanapoingia kwenye viwanja vya ndege vya Afrika Kusini.