Mkuu wa Wilaya wa Temeke, Jokate Mwegelo
DC Jokate ameyasema hayo leo, huku akieleza kuwa vijana hao wamekamatwa katika msako wa polisi ulioanza Septemba 14, 2022, huku akisisitiza kuwa msakao mkali unaendelea.
Aidha DC Jokate amebainisha kuwa serikali haitamvumilia yoyote anayejihusisha na vitendo hivyo vya uhalifu, huku akitoa tahadhari kwa baadhi ya vijana ambao hushinda vijiweni pasipo kujishughulisha na kazi yoyote.
Wiki hii katika wilaya ya Temeke yameripotiwa matukio ya panya road katika kata tatu za Chamazi, Kilungule na Mianzini.

