Jumatatu , 7th Dec , 2020

Kuelekea msimu wa Sikukuu za mwishoni mwa mwaka benki ya NCBA imetangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja wake watakaonunua bidhaa katika maduka ya GSM.

Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi NCBA na kulia ni Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Utaifa wa Benki hiyo, Caroline Mbaga

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi NCBA Julius Konyani amesema punguzo hilo ni kwa wateja wote ambao watanunua bidhaa katika maduka ya GSM kuanzia kiasi cha shilingi laki moja na nusu.

Naye Ofisa Masoko wa GSM, Fatma Farah amesema wamejipanga vizuri kutoa huduma hiyo ambapo pia amewakaribisha wateja hao katika maduka yao.