Jumanne , 24th Nov , 2020

Katibu Mkuu wa Bavicha Nusrat Hanje, na mratibu wa uhamasishaji  Twaha Mwaipaja, wameachiwa huru pamoja na wenzao sita baada ya kufutiwa mashtaka dhidi ya kesi iliyo kuwa inawakabili katika Mahakama ya mkoa wa Singida.

Pichani Ofisi ya Chadema

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) watuhumiwa hao waliachiwa siku ya jana tarehe 23/11/2020 usiku huku wakitaja sababu yakuachiwa kuwa  upande wa Jamhuri  haupo tayari kuendelea na kesi hiyo.

Nusrat Hanje, Mwaipaya pamoja na wenzao sita walikuwa wanakabiliwa na  tuhuma zakufanya mikusanyiko isiyo ya halali , kudharua wimbo na bendera ya taifa .

Aidha kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA wanasiasa hao wanaachiwa huru wakiwa wametimiza siku 133 Gerezani huku  wakiachiwa huru kabla ya maamuzi ya rufaa yao ambayo ilitakiwa isikilizwe tarehe 25/11/2020.