Ijumaa , 24th Jul , 2015

Baada ya kujipanga vyema katika kazi za uongozaji wa video za wasanii mbalimbali jijini Dar es Salaam muongozaji mahiri Abbas Adam leo anaitambulisha kazi mpya ya msanii wa muziki wa Bongofleva nchini Nedy Music kupitia kipindi cha FNL cha EATV.

muongozaji mahiri wa video za wasanii nchini Abbas Adam

Abbas Adam ameiambia eNewz kuwa kazi hii iliyobatizwa jina 'Dayana' ni kazi mpya ambayo imetayarishwa chini ya MAc Media huku upande wa audio ikifanywa na Bob Manecky, ambapo kupitia eNewz unaweza kuona jinsi matayarisho ya kazi hiyo behind the scene ilivyochukua nafasi yake.