"Akipata 'Division One' nampa Insta yangu" - Nisha

Jumatatu , 1st Mar , 2021

Kumekuwa na utaratibu kwa mzazi kumuahidi vitu mtoto wake kama njia ya kumshawishi ili afanye vizuri kwenye masomo, sasa msanii wa filamu Nisha Bebe ametoa kali ya mwaka kwa kusema mtoto wake akipata 'Division One' atampa akaunti yake ya mtandao wa Instagram.

Msanii wa filamu Nisha Bebe

Nisha Bebe amesema ana mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 16 na yupo kidato cha nne kwa sasa, hivyo ametumia njia hiyo kumpa nguvu kwenye masomo yake ili asiwe na vishawishi vingine, tamaa au ustaa ambavyo vitaharibu masomo yake.

"Mimi mtoto wangu hakuna mtu anayemjua ana miaka 16 yupo 'form four' hata shule watu hawajui anasoma wapi na nimeamua kuishi nae hivyo mpaka akifikisha miaka 18 ndiyo nitampost, nimemwambia akipata division one ya 7, nampa page yangu ya Instagram inakuwa ya kwake na jina nabadilisha" ameeleza Nisha Bebe

Tazama hapa akizungumzia suala hilo.