Jumatatu , 18th Aug , 2014

Msanii wa muziki wa kimataifa, Alaine kutoka nchini Jamaica anatarajiwa kumwaga mvua ya burudani nchini Kenya siku ya Tarehe 6 mwezi Septemba mwaka huu.

msanii wa muziki wa nchini Jamaica Alaine

Kuhusiana na ujio huu ambao unasubiriwa kwa hamu katika sehemu mbalimbali nchini Kenya, Alaine mwenyewe kwa njia ya mtandao amewataka mashabiki wake kukaa tayari kukutana naye siku ya tukio.

Alaine pia ametumia neno la Kiswahili Nakupenda Pia kutoka kolabo yake na Wyre na kuelezea mapenzi yake kwa chakula maarufu cha Chapati ambacho pia kinapatikana Afrika Mashariki.

msanii wa muziki, Jamaica, Alaine