Alhamisi , 13th Oct , 2016

Meneja wa Band ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, amefunguka na kusema kuwa anataka amrudishe msanii wake mmoja kati ya wasanii wake wa zamani ambao walikuwemo kwenye band hiyo.

Asha Baraka

Akiongea na eNewz alisema kuwa anataka kumrudisha msanii huyo (Bila kumtaja jina) kwa madai kuwa yeye ndiye aliyemtengeneza hadi kufikia hapo alipo

“Nikimaliza zoezi langu la kurudisha wasanii ambapo waliporwa kwenye band yangu wale ambao niliwatengeneza mimi basi nitaanza kusajili wasanii wachanga wanaoanzia miaka 18 na kuendelea na msanii aliyebaki ni mmoja tu ila siwezi kumtaja kwa sasa ila siku ikifika basi nitamtaja” Alisema Asha Baraka

Alimalizia kwa kuomba vyombo vya habari viweze kuunga mkono muziki wa band nchini kwa sababu bado muziki huo unafanya vizuri