Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Aslay na Nandy kupelekwa Mahakamani

Jumatatu , 12th Feb , 2018

Wasanii wa kizazi kipya Aslay pamoja na mwanadada Nandy wanaoendelea kufanya vizuri na kibao chao cha 'Subalkheri mpenzi' wanatarajiwa kuburuzwa Mahakamani kutoka na kuimba wimbo huo bila ya ridhaa ya wahusika.

Hayo yameibuka baada ya mmiliki wa wimbo huo, Kikundi cha Tarab Asilia visiwani Zanzibar (Culture Music  Club) kudai pesa zilizotolewa jumla ya Tsh. 800,000 kama fidia za kutumia kazi hiyo hawazitambui hivyo wanajipanga kuwapeleka mbele ya Mahakama.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa kikundi hicho, Taimur Rukuni Twaha, amesema wasanii hao kabla ya kuimba tena upya wimbo huo walipaswa kuonana na uongozi huo ili kukubaliana jambo ambalo hawakufanya hivyo.

"Walichokifanya Aslay na Nandy kwenda kwa waimbaji wetu na kuwapa kiwango hicho cha fedha kwetu tunaona hakikubaliki na wametoa kama zawadi tu kwa sababu thamani ya wimbo wetu haulingani na kiwango hicho. Kwa mujibu wa katiba ya kikundi chetu, ibara ya sita inaeleza nyimbo zote zilizoimbwa na kikundi ni mali ya kikundi na kwamba muimbaji, mtunzi na muweka sauti watakuwa na haki zao kupitia kikundi hicho", amesema Twaha.

Kwa upande mwingine, Twaha amesema msimamo wao utabaki pale pale wa kuwafikisha Mahakamani wasanii hao endapo watashindwa kutimiza masharti waliyopewa na uongozi wa kikundi hicho.

Chanzo: Nipashe

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali