
Rama Dee (Kushoto), AT (Kulia)
Hayo yamekuja siku chache baada ya msanii Rama Dee kusema kiwango cha ‘director’ Mkongwe Adam Juma kiko chini ya viwango katika kutayarisha na kutengeneza ‘video’ na kwamba anamtaka ajifunze kutoka kwa Hanscana.
“Imekuwa desturi kwenye nchi yetu mtu kutomuheshimu mwenzake au nguvu zake, leo unatoka unasema Adam Juma hajui ku-shoot ‘video’, wakati wewe ukipewa ile kamera hata kupiga picha huwezi kujua lakini yule mtu ndiyo amekuja muziki wa Tanzania”. Alisema AT kupitia kipindi cha eNewz cha EATV
Aidha msanii huyo amesema wasanii ndiyo wanaongoza kwa kutokuwa na heshima, hivyo amewataka wasanii wenzake kuwa na heshima kwa watu waliowazidi.