Alhamisi , 8th Sep , 2016

Kundi la The Heroes ambalo lilishiriki Dance100% kwa mara ya tatu mwaka huu na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na hatimaye kushindwa kufuzu fainali limesema litaimarisha kundi lao ili kuendelea kushiriki kazi nyingine .

Kundi la The Heroes

Akizungumza na EATV kwa niaba ya mwenzake Emmanuel Dickson amesema wameshiriki mara ya tatu hivyo wameweza kujenga umoja hadi sasa na ndiyo maana mwaka huu wakaweza kushiriki bila tatizo.

“Tumeshiriki mara ya tatu na hata baada ya kushindwa, sisi shughuli zetu tunafanyia Gongo la Mboto na tutaendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali na ikitokea tukio bado tutafanya na tutajipanga vya kutosha Dance100% ijayo” Amesema Emmanuel.

Shindano la Dance100% limefikia hatua ya fainali mbapo makundi kwa sasa yanaendelea na maandalizi, ambapo yatachuana makundi matano yaliyoshinda hatua ya nusu fainali ili kundi moja liweze kuibuka na ushindi.

Kundi litakaloibuka na ushindi mwaka huu kuibuka na kitita cha milioni 7 ambapo shindano linadhaminiwa na Vodacom na Coca Cola na kuoneshwa na EATV kila Jumapili saa moja Jioni.

Tags: