Jumapili , 15th Feb , 2015

Baba mzazi wa msanii wa muziki Dully Sykes, Mzee Abby Sykes amefariki dunia katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Marehemu Mzee Abby Sykes

Sababu ya kifo cha mzee Sykes imeelezwa kuwa ni vidonda katika miguu ambavyo vimekuwa vikimsumbua kwa takriban miezi minne bila kupona na kusambaza sumu sehemu nyingine za mwili na hatimaye kusababisha kifo chake.

Mzee huyo ambaye alikuwa kivutio cha wengi hasa kutokana na uwezo wake mkubwa katika kuimba na kupiga gitaa na muonekano wake wa ujana zaidi, anakuwa ni pigo jingine kubwa katika tasnia ya Burudani katika upande wa muziki.

Mastaa mbalimbali wameendelea kutuma salamu zao za pole kwa njia ya mtandao kufuatia taarifa za msiba huo ambapo mpaka sasa tunafuatilia taarifa za chanzo cha kifo cha mzee Sykes.

eNewz tunamtakia Dully Sykes pamoja na familia nzima na wale wote wanaoguswa na msiba huo faraja na pole na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Aamin.