Baba wa watoto 151,wake 16 aapa kuongeza familia

Jumanne , 11th Mei , 2021

Hii ndiyo maana halisi ya maskini furaha yake ni watoto wake na familia yake, huko nchini Zimbabwe mzee wa miaka Misheck Nyandoro mwenye watoto 151 na wake 16 amesema bado ana mpango wa kuongeza wanawake wengine na watoto wengine.

Picha ya Mzee Misheck Nyandoro na watoto wake

Mzee huyo wa miaka 66 amesema ameanza style hiyo ya kuoa wake wengi kuanzia 1983 amesema ndoto yake ni kuwa na wake 100 na watoto elfu 1, na ndoa yake ya 17 itafanyika majira ya kiangazi.

"Ninachofanya ni kumalizia project yangu niliyoanzisha mwaka 1983, sitaacha mpaka kifo kinichukue, sasa hivi najiandaa na ndoa yangu ya 17 itafanyika majira ya kiangazi, watoto wangu wananisaidia wananipa pesa na zawadi

"Kila mmoja wa wake zangu hunipikia kila siku, lakini kanuni ni kwamba mimi hula chakula kitamu tu, ambacho nitaona chini ya kawaida hutupiliwa mbali wanajua sheria, waliahidi kutokasirika wakati nitapeleka chakula chao kwao. Chochote kinachorudishwa kinapaswa kuwa somo linalowasaidia kuboresha" ameongeza

Aidha mzee huyo amesema kwa usiku mmoja hutumia angalau kulala na wake zake wanne kati ya 16 kwa usiku mmoja.

Chanzo : Fr24 New na Tuko News.

Jionee Ugomvi wa Nay wa Mitego na Mama mtoto wake, bonyeza hapa kutazama