Banana awaacha watoto wake wenyewe

Thursday , 7th Dec , 2017

Umaarufu wa msanii usiulete  katika familia  acha watoto wachague wenyewe, hayo amesema leo msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Banana Zoro katika "interview" na East Africa Radio.

"Umaarufu  ni gharama, watoto wangu nawaacha wachague wenyewe kipi wanataka wafanye,wachague umaarufu wa maisha ya kawaida, ila kitu cha kwanza lazima tuwaelekeze katika elimu",amesema

Banana Zorro ni msanii ambaye hana mambo mengi katika maisha yake ya usanii, hachanganyi kati ya usanii na familia.

"Unapochanganya familia na usanii unaweza kuharibu mfumo mzima wafamilia , usichanganye vitu hivi". Banana amesema.

Banana  Zoro ambaye amezaliwa katika familia ya muziki,amewahi kutamba na ngoma kali  kama vile Mama yangu,Nzela aliyoimba na bendi yake ya B-band na Mapenzi gani.