Barnaba aeleza kitu anachochukia mwilini mwake

Jumatano , 7th Aug , 2019

Leo tumepiga stori na msanii Barnaba Classic na amezungumzia suala la mastaa wengi kutohudumia familia zao pamoja na kitu ambacho hapendi kufanya tena kwenye mwili wake.

Barnaba amefunguka hayo kupitia EATV/Radio Digital alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutohudumia familia yake ambapo amesema,“kwa upande wangu familia yangu sio maonyesho, sio sehemu kila mtu ajue ninachokifanya, si nguo kila mtu akanunua au akavaa mambo mengine hayawahusu ila watoto wangu wapo vizuri", amesema Barnaba.

"Kuhusu Mama Steve, kama nimewasiliana nae au watoto watu wanaongea tu hawajui au kwa sababu Barnaba ni staa”, ameongeza.

Pia Barnaba amesema ana michoro mitano kwenye mwili wake, ila kwa sasa anazichukia sana na hafikirii kuongeza michoro mingine kwa sababu ameshakuwa mzazi na hayo ni mambo ya ujana.