Barnaba amtaka msanii aache pombe

Jumatatu , 5th Aug , 2019

Leo tumepiga stori na msanii wa BongoFleva Barnaba Classic, ameeleza mambo mengi ikiwemo Familia yake, Lebo ya muziki, T.HT., Lifestyle pamoja na kutoa ushauri kwa wasanii wa kike.

Barnaba Classic

Barnaba Classic ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital na kutoa ushauri kwa wasanii wa kike kama Amber Lulu na Amber Rutty kwa kufanya vitu vya kukosa maadili.

"Wajitambue na watambue nafasi zao katika Jamii kwa sababu sanaa sio kukaa uchi, kuhusu Amber Lulu ni kuendelea kumsihi kama dada yangu ajaribu kurudi najua anaanguka, anajikwaa najaribu kumsihi apunguze pombe ili kulinda maadili".

Aidha msanii huyo ameendelea kueleza kuhusu nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (T.H.T), haijafa kama watu wanavyosema, ila kuna ukarabati unaendelea na kuanzia tarehe 19 itazinduliwa tena.

Pia Barnaba Classic amewajibu wanaombeza kuwa hajatoboa kwenye muziki upande wa kimataifa kwa kusema, bado anaamini kwenye muziki mzuri japo watu wanamsema hajavuka soko la kimataifa wala haoni maana ila wanatakiwa waheshimu uwepo wake kwenye muziki.