Beka Flavour amjibu Aslay

Saturday , 12th Aug , 2017

Msanii Beka Flavour ambaye ni moja ya wasanii wanaounda kundi la Yamoto Band amejibu mashambulizi ya kuachia ngoma ndani ya muda mfupi kama ambavyo msanii mwenzake kutoka katika kundi hilo Aslay amekuwa akifanya. 

Beka Flavour ameachia ngoma yake inayofahamika kwa jina la 'Sikinai' miezi miwili kupita toka ameachia wimbo wake 'Libebe' baada ya wasanii hao kuanza kufanya kazi za peke yao nje ya kundi lao la Yamoto Band.

Wasanii hao Beka Flavour na Aslay ni kati ya wasanii ambao tayari wameonyesha kushindana katika kazi huku kila mmoja akitaka kuonyesha uwezo wake kimuziki na kufika mbali zaidi kupitia kazi zao. Kwa upande wa Aslay ndani ya miezi minee toka wasanii hao waanze kufanya kazi za peke yao ameweza kuachia video tano mfululizo, huku wasanii wengine wa kundi hilo akiwepo Maromboso pamoja na Enock Bella wakiwa kimya mpaka sasa wakijipanga. 

Tazama video mpya wa Beka Flavour hapa