Jumatano , 14th Jan , 2015

Wasanii wa muziki kutoka orodha iliyosheheni wakali watakaofanya onesho kali katika tamasha la tiGO Kiboko Yao tarehe 24 mwezi huu Leaders Club Jijini Dar es Salaam, wameonesha msisimko wa aina yake katika siku ya onesho.

Msanii wa muziki wa dansi nchini Tanzania Christian Bella

Katika mahojiano binafsi na eNewz, msanii wa muziki Christian Bella, Isha Mashauzi kati ya wengine kibao, wamewataka mashabiki wao kukaa tayari kwa kushuhudia nguvu na upya wa burudani, katika tamasha hilo lenye hadhi ya kimataifa la tiGO Kiboko Yao ikiwa ni onesho lao kubwa kabisa la kuanzia mwaka.