Jumatano , 1st Apr , 2015

Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi nchini kutoka bendi maarufu ya malaika Band, Christian Bella leo hii ametoa zawadi kwa mashabiki wake kwa kutambulisha kichupa chake kipya hapa EATV alichokibatiza jina 'Nashindwa'.

Mwanamuziki wa bendi ya Malaika nchini Christian Bella

Bella ameongea na eNewz kuwa kichupa ambacho kimefanyiwa kazi nchini Afrika Kusini ni moja kati ya video zake aliyotumia kiasi kikubwa cha pesa kugharamia kazi nzima ambapo pia amegusia juu ya maana ya ujumbe uliomo na mipango inayofuata ikiwa ni maandalizi ya tarehe rasmi ya kuizindua video hiyo.