Jumatano , 23rd Sep , 2015

Star wa muziki wa dansi nchini Christian Bella Obama a.k.a King of the Best Melody hivi sasa amejipanga kusafiri nje ya nchi kukamilisha mpango wa kufanya kolabo na moja ya wasanii wakubwa kabisa barani Afrika.

Staa wa muziki wa dansi nchini Christian Bella Obama aka King of the Best Melody

Bella a.k.a CB Reezy baada ya kufanya ziara kubwa ya muziki mikoani inayoitwa 'Amerudi Tour' amesema ni mapema mno kumtaja star huyo ambaye anajipanga kufanya naye kazi, amesema pia kuwa katika kipindi hiki anafurahi sana kuona kuwa kazi yake ya 'Amerudi' ikiwa imepokelewa vizuri kila kona.

Star huyo pia ameeelezea kuwa anaendelea pia kupiga hatua kubwa kuimarisha kikosi chake kwa kutambulisha marapa wawili wapya na pia mwalimu wa dansi katika bendi yake ya Malaika.