Ijumaa , 24th Apr , 2015

Staa wa muziki Ben Pol, leo hii ikiwa ni siku tatu tangu kutoka rasmi kwa video yake ya SOPHIA, ameweka wazi kuwa anajisikia vizuri kuona malengo yake na ujumbe aliopania kuufikisha kupitia video hiyo, ukiwa umefika.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Ben Pol

Staa huyo wa muziki ameweka wazi kuwa, hii ndiyo video yake ya kwanza kupata mapokezi makubwa na watazamaji wengi kwa siku za awali katika mtandao, taarifa za chini ya kapeti pia zikiweka wazi uwezekano wa msanii huyo kuanza kufanya kazi na mashirika ya utetezi wa walemavu wa ngozi kutokana na kazi hiyo.