Jumatano , 2nd Dec , 2020

Baada ya msanii Marioo kumpa heshima Aslay Isihaka sasa ni zamu ya msanii Ben Pol ambaye amemtumia ujumbe mzito Barnaba Classic kuhusu anachokifanya na uwepo wake kwenye muziki wa BongoFleva.

Kulia ni Ben Pol, kushoto ni Barnaba Classic

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Ben Pol ameandika kuwa

"Siku ya tatu leo nimekuwa nikifikiria jinsi ya kumuandika huyu mwamba, leo nimesema sitaki kupatia kuandika, nataka niandike hivyo hivyo ninavyojisikia kuhusu yeye, kwanza amefanya hit songs zisizopungua 300 za kwake mwenyewe, za kuandikia wengine na zile za kuchangia uandishi kwa watu

"Ame-inspire wasanii wengi mno! hata kama wengine hawatasema leo, Mimi mwenyewe nishawahi kuwa namsindikiza siku hizi wanaitwa Chawa, enzi hizo akienda studio kwa Allan Mapigo Masaki ili mradi tu awe ananifundisha maujanja yake ya kuimba na kutunga

"Ifike mahali watu wapewe maua yao wanayostahili, mapeema wayanuse wenyewe kabla haijawa too late wakiwa hawapo. Kaka wewe ni Chuma cha muziki kweli kweli!!. Halafu huna choyo, unaamini na kuwasaidia binadamu wenzako haraka mno bila hata kujiuliza" ameongeza