Jumatano , 10th Jun , 2015

Ben Pol, Msanii wa muziki ambaye amepiga hatua ya ziada kuweka muziki wake katika mitandao ya kimataifa ya kuuza muziki, ameeleza namna hatua hiyo inavyosaidia kuwafikishia kazi zake mashabiki kwa mara moja.

Msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Ben Pol aka Baba Sophia

Ben ama Baba Sophia kama anavyojiita mwenyewe sasa, amesema kuwa, kutokana na nafasi hiyo kwa upande wa msanii binafsi, anaweza kuivusha sanaa yake mipaka kwa kujua ni katika eneo gani duniani kuna mashabiki wake ama uhitaji zaidi wa kazi zake kwa ajili ya kwenda kufanya show.

Vilevile kwa mujibu wa msanii huyu, nafasi hii pia ni utambulisho mzuri kwa msanii kutokana na jukwaa la mtandao kuendelea kukua siku hadi siku kujua ni wapi wanapenda kazi zake zaidi na pia kuongeza kipato.