Jumanne , 26th Jan , 2016

Msanii wa muziki Ben Pol, amesema kuwa wigo wa muziki wake umeongezeka kwa kiasi kikubwa, baada ya kufanikisha kuingiza katika mzunguko Video ya rekodi yake ya 'Ningefanyaje' ambayo ni ya kwanza kwake kuifanya katika kiwango cha kimataifa.

Ben Pol

Ben Pol amesema kuwa, nafasi ambayo rekodi hiyo imepata katika chati za kimataifa, imemuwezesha kukaa katika mstari na kueleweka na wasanii wakubwa, kutoka Nigeria na nchi nyingine akiwa sasa ana mkakati wa miezi 3 mbele kupiga hatua kubwa zaidi kimuziki.

Ben Pol amesema kuwa, baada ya kuthubutu na kufanya uwekezaji mkubwa kwa kazi hiyo, amekuwa ni msani mwenye mikakati ya mbele, kama ambavyo wasanii wengine wakubwa wa kimataifa wanavyoendesha sanaa zao, lengo likiwa ni kusonga mbele na kufanya kazi ambayo itafunika ile ambayo ipo katika mzunguko sasa.