Ijumaa , 12th Sep , 2014

Wasanii wa muziki Ben Pol pamoja na Shaa, kwa nyakati tofauti wamezungumza juu ya umuhimu wa kuuamsha muziki wanaoufanya kwa kuupiga live wakiwa na bendi, hatua ambayo wamesema mara nyingi inakwamishwa na bajeti ndogo za waandaaji wa maonyesho.

msanii wa muziki wa RnB na bongofleva Ben Pol

Kwa upande wa Ben Pol, staa huyu amesema kuwa yeye hufanya onyesho la muziki kulingana na muandaaji anavyojipanga, na ambapo atatakiwa kufanya muziki live basi hukodisha bendi ili kufanikisha.

Kwa upande wa Shaa, mwanadada huyu amesema kuwa mara nyingi waandaaji wa maonyesho ndio wanaosababisha wasanii kuimba kwa playback.

eNewz imeongea na wakali hawa kuhusiana na umuhimu wa kupiga muziki wa Live.