Jumatano , 20th Mar , 2019

Mwanamuziki mwenye umri mkubwa zaidi kwenye game ya bongo fleva, Bi. Cheka, ameweka wazi hali yake kiafya kuwa si nzuri, na kwamba anahitaji msaada wa Watanzania kuweza kumudu gharama za matibabu.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Bi. Cheka amesema kwa sasa anasumbuliwa sana na tatizo la moyo, na dawa anazotumia ni ghali sana, hivyo anaomba msaada wa Watanzania kuweza kuzipata.

Akiendelea kuzungumzia hilo Bi Cheka amewataka watu hata akifa waende kwa wingi wakaamzike, kwani anawapenda sana.

Aelezea machungu yake

“Moyo unaenda mbio, mara nyingine nakosa nguvu, kuna tatizo la moyo tu unaniuma, dawa kopo linauzwa laki moja, na linatumika ndani ya miezi miwili, kila siku kimoja, hizi dawa zimetoka Ugiriki alikofia mtoto wangu, ndio marafiki zake wakasema tumchukulie mama, ila hapa nimetafuta sana hamna”, amesema Bibi Cheka.

Bibi Cheka pia ameomba msaada kwa Watanzania kwa chochote kama kuna ambaye atapenda kumchangia.